NICE HAIR! Vyakula bora kwa nywele yenye afya .Fahamu unachohitaji kula kwa nywele nzuri

Hair
Hair
Kitu cha kwanza ambacho  hukutangaza kama mtu ni nywele ,na hasa kwa akina dada . ni muhimu kufahamu jinsi unavyoweza kuwa na  nywele ndefu  na yenye afya kutumia vyakula bora ambavyo vitakunufasha kuboresha afya ya nywele yako . Kando na mafuta na kemikali nyingi zinazotumiwa kwa ukuuzaji na utunzi wa nywele ,vyakula hivi pia ni muhimu sana na havina madhara ya kando ambayo hutokana na matumizi ya kemikali au mafuta ya kutunza nywele .

1.  Mayai

Mayai ni  kitovu muhimu cha protini na biotin  ,virutubiusho muimu sana katika ukuaji wa nywele . kula protini ya kiasi kifaacho  ni muhimu kwa ukuaji wa nywele .ukosefu wa protini umefahamika kusababisha kupotea kwa nywele . biotin ni muhimu sana kwa utenezaji w protini muhimu kwa jina keratin .

2.Tunda dogo/ Berries

Matunda madogo ya Berries  yamejaa  viungo na vitamini muhimu vya kuwezesha ukuaji wa nywele . vitamin hizo ni pamoja na  Vitamin C  . Mwili huyumia vitamin C  kutengeza kiungo cha collagen  ,protini ambayo hufanya nywele kuwa thabiti  na kuizuia kuchanika  .  Vitamin C pia huusaidia mwili kupata madini ya chuma au Iron kutoka kwa vyakula .uhaba wa Iron husababisha ugonjwa wa Anaemia ambao husababisha kupotea kwa nywele .

3. Spinach

Mboga ya spinach  ina madini muhimu sana yanayowezesha ngozi kutoa unyevu  na vitamin A na C  ambazo husaidia ktika ukuaji wa nywele . ufuta maalum kwa jina  Sebum hutolewa na ngozi ya kichwa ili kusaidia katika ukuaji wa nywele . Gramu 30 za spinach hutoa takriban aislimia 54 ya mahitaji yako ya kila siku ya Vitamin A .

4. Samaki wa ufuta

Samaki wenye ufuta kama vile   Chache au salmon  husaidia katika ukuaji wa nywele .samaki hao hutoa omega 3 ambazo ni aside zinazohusishwa na ukuaji wa nywele . Mafuta ya samaki pia huzuia kupotea kwa nywele  na kuongeza ukuaji wa nywele kwa wanawake .

5.  Viazi vitamu

Viazi vitamu ni  muhimu sana kwa  madini ya  beta-carotene.  Mwili hubadilisha kiungo hiki muhimu kuwa Vitamin A  ambavyo vinahusishwa na afya nzuri ya nywele . Kiazi kimoja kitamu  kina takriban gramu 114  za beta carotene  inayoweza kukupa vitamin A mara nne zaidi ya mahitaji yako ya kila siku .

6. Parachichi/Avocados

Avocados  ni tamu sana na zina  mafuta ya jani ya kiasini ambayo yana vitamin E inayosaidia sana katika ukuaji wa nywele .Vitamin E pia hulinda sehemu ya ngozi  kama vile  nyozi ya ufuvu wa kichwa . avaocado pia zina aside  maalum yenye mafuta  ambayo huzuia nyewele kupotea . Vyakula vingine muhimu katika ukuaji wa nywele yenyeafya ni Njugu ,Pilipili tamu ,chaza/Oysters,uduvi/shrimp,maharagwe,soya  na nyama.