16508539_686417551538056_4275234156423186793_n

‘Nikifa wacha mafans wangu wanipost,’ Mcheshi Zeddy asema

Mcheshi wa Churchill Live Zainabu Zeddy amegadhabishwa na kitendo ambacho wasanii wengi hutelekezwa wangali hai na wakifa wanapendwa na kila mtu kuwaomboleza.

Zeddy aliweka mambo wazi na kusema kuwa kama huwezi msaidia mtu akiwa hai kuna haja gani kumsifu akiwa mauti na kuonyesha upendo kwake.

Premonition? Zeddy alizungumzia kifo cha Kasee miezi,8, iliyopita

20200629_071826-696x474

“kama huezi nisaidia nikiwa hai nikifa achana na mimi kabisa 😥usiwai ni post acha Mafans wangu wanipost.”

Zeddy aliyeonekana kugadhabishwa alisema kuwa unafiki huo ukizidi atafichua majina na picha za watu ambao wanafanya wasanii wengi kuwa na msongo wa mawazo na kuchangia vifo vyao.

“Hehe Yaani kila Msanii naona post Rip Kasee! Wanafiq nyinyi it’s high time hii ufala iishe!! kama huezi nisaidia nikiwa hai nikifa achana na mimi kabsa!😥usiwai ni post acha Mafans wangu wanipost ata hivyo sijawai ona mtu amekulwa na umbwa ati amekosa wa kumzika!Yarabb tuepushe🙏kufa ni lazima lakini hii ya “Comedians”imezidi. ni vizuri watu wajue nini hukula wasanii wakafikia kujitoa uhai kwa next post nakam na majina na picha zao,lazima tukomeshe unyanyasaji dhidi ya Wasanii.#wasaniiwaacheuoga #Depression#victimization.” Aliandika Zeddy.

SIZk9kpTURBXy8zMjgyY2VmODE1YjI5ZWQ1MDhkZTBiOWY0NjI0OTJlNS5qcGeRkwXNAxTNAbyBoTAB

Usemi wake unajiri wakati ndugu, jamaa na marafiki wanaomboleza kifo cha mcheshi ‘Kasee’ aliyepatikana barabarani akiwa ameaga, kiini cha kifo chake bado hakijabainika.

 

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments