Niko tayari kuendeleza historia ya Gor Mahia - David Mapigano

david.mapigano
david.mapigano

Mlinda lango mpya wa Gor Mahia, David Mapigano anasema nia yake ni kushinda mataji na mabingwa hao wa KPL na kuendeleza historia nzuri ya klabu hio. Mzaliwa huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 26 alijiunga na KO’galo msimu huu na amecheza mechi tano tayari.

Gor itaanza utetezi wa ligi dhidi ya Tusker hii leo katika uwanja wa Kisumu.

Miamba wa Uingereza Manchester United watacheza na Partizan Belgrade, AJ Alkmaar na Astana katika kundi L ya kombe la Uropa.

Katika droo iliyofanywa Monaco Ufaransa Ijumaa, Arsenali ambao owalipoteza katika fainali ya mwaka jana dhidi ya Chelsea watacheza na Vitoria SC, Frankfurt na Standard Liege katika kunci F.

Wolves pia ya Uingereza itacheza na Besiktas, Braga na Bratislava katika kundi K. Mabingwa mara tatu kwa mpigo Sevilla watachuana na  Dudelange, APOEL na Qarabag  katika kundi A.

Mechi za kwanza zitachezwa Septemba tarehe 19. Vile vile, mshambulizi wa zamani wa Chelsea Eden Hazard alituzwa kama mchezaji bora wa ligi ya Uropa msimu wa 2018/19.

Mlinzi wa Manchester United defender Chris Smalling amewasili Italia kumalizia mazungumzo ya kujiunga na klabu ya Roma kwa mkopo.

Miamba wa Uingereza, United wamekubaliana na Roma kitita cha pauni million 2.7, kwa huduma za muingereza huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye alijiunga nao kutoka Fulham mwaka wa 2010. Smalling aliongeza kandarasi yake ya Old Trafford hadi 2022.