eliud

Niko tayari kujaza nafasi ya Ken Okoth – Eliud Owalo

Leo asubuhi katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi, bwana Ghost Mulee alikuwa mwenyeji wake mgombea wa kiti cha ubunge cha Kibra, bwana Eliud Owalo.

Bwana Owalo anawania kuwa mbunge katika ngome inayo aminika kuwa ya aliyekuwa mbunge wa Lang’ata, mheshimiwa Raila Odinga, kupitia tikiti ya chama cha ANC kinacho ongozwa na bwana Musalia Mudavadi.

Daah! Fred Omondi afunguka na kusema ameokoka

Kulingana na Owalo, anajua hatua ya kuijaza pengo iliyowachwa na marehemu Ken Okoth itakuwa ngumu lakini anaamini kuwa ana maarifa na ujuzi wa kupeleka Kibra mbele.

Bwana Okoth aliaga dunia mwezi wa Julai mwaka huu baada ya kuugua saratani.

“Agenda yangu kwa wakazi wa Kibra ni kufanya kitu kiitwacho Radical transformation agenda. Kwa mfano ukosefi wa Karo ni shida kubwa sana na nitaimarisha kiwango cha bursary kutoka elfu 5 kwa mwanafunzi hadi elfu 10.” Alisema Owalo huku akisisitiza, heri tufunze wachache lakini wasome hadi mwisho ili waje wasaidie wenzao.

Kitu kingine anachopania kushughulikia akiibuka mshindi katika uchaguzi huo mdogo utakaofanyika tarehe saba mwezi Novemba ni swala la moto ambao umekuwa ukiwahangaisha wananchi wa eneo hilo.

Anasema nia yake ni kutafuta wafadhili ili wanunue magari au mashine za kupambana na moto badala ya kutegemea magari ya kaunti ya Nairobi.

Changamoto kuu linalokumba wakazi wa Kibra, kulingana na Owalo ni ukosefu wa ajira kwa vijana na kina mama.

Nitahakikisha wadi zote zina afisi za kuwasaidia vijana kutafuta kazi. Kutakuwa na data base ambayo itatumika kuwaunganisha vijana na nafsi za kazi kulingana na uwezo au masomo au ustadi wao.

Wanawake single mothers tutawasaidia waanzishe biashara hata kama ni kuuza samaki au mboga Kwani wakisaidika watasaidia familia nzima.

Ronaldo afunga mabao 4 huku Ureno wakiwanyuka Lithuania 1-5

Hata hivyo, licha yake kuwa mwandani wa bwana Raila miaka kadhaa katika chama cha ODM, bwana Owalo anaamini kuwa hatua yake ya kujiunga na ANC ni kufuatia kutoridhishwa kwake na jinsi uchaguzi wa nominations ziliendeshwa hapo awali.

Nilifanyia ODM miaka Sita baada ya kuiwacha Kazi yangu ambayo sikuwa nalipwa lakini sikufurahishwa na nominations. Kama wanavyosema yaliyopita si ndwele tugange yajayo.

Owalo anasema licha yake kutokuwa mbunge wa Kibra, amefanya juhudi za kuwapeleka vijana takriban 1000 kwa shule ya uendeshaji gari kwa kutumia fedha zake.

Anasema furaha yake kuu ni kuwa alipatana na mmoja wa vijana wale, ambaye sasa yeye ni dereva wa balozi.

Yote tisa, kumi ni kuwa mheshimiwa Owalo aliapa kuendeleza kazi nzuri aliyoifanya bwana Ken Okoth kwani ana imani kuwa mda umefika wa kuwacha siasa za kuharibu kazi njema iliyofanywa na waheshimiwa wa awali.

Wakati nilikuwa napambana na bwana Okoth nilimwambia wacha mashindano yetu yawe kuhusu sera, na Okoth ni mmoja wa wa Bunge waliofanya Kazi njema kwa mda wa miaka kumi iliyoisha humu nchini.

Lazima tubadilishe siasa, Sio eti ukiingia uongozini eti unamaliza mipango ya aliyekuwa mbunge wa eneo fulani.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments