'Niliambiwa niko na sauti iko na homa,'Msanii Kidum aeleza jinsi alifukuzwa kwaya

Msanii Kidum amefichua jinsi alifukuzwa kutoka kwa kwaya baada ya msimamizi wa kwaya kumwambia kuwa hana sauti ya kuimba na jambo ambalo lilimuathiri maishani mwake.
"Kwa kwaya niliwahi kufukuzwa… niliambiwa siwezi imba nilifukuzwa kwa sababu ilikuwa ni ya kanisa la katoliki na huyo Mzungu mwenye alikuwa anatufundisha sisi watoto kuimba alinimbia kwamba niko na sauti mbaya na kuniathiri sana

Niliambiwa niko na sauti iko na homa homa hivi, nikapata mzee mwingine wa kunifunza Gita ndio akajenga ujasiri wangu tena aliniammbia sauti yoyote yaweza kuimba muhimu ni kujua kutumia sauti yako." Alisema Kidum.

Kidum ameishi humu nchini kwa miaka,25, alikuja nchini baada ya vita kuzuka nchini Burundi.

“Mimi nimekaa miaka 25 Kenya na umri niko na 46 years, na hapa Kenya sikai tu, niko na jamii yangu, na hata watoto wanapozaliwa wanajua hapa ndo kwao. Nishawahi fanya attempt yakwamba mimi ni kutoka Burundi, so Burundi wataiaccept kama kwao lakini ikashindikana, coz walizaliwa hapa."