Nilianza na kazi ya mjengo kabla ya kuwa muigizaji - Bernard Otieno

bernard otieno
bernard otieno
Bernard Otieno Kijana wa miaka 25 ni mcheshi ambaye safari yake hadi kuwa muigizaji ni ya kushangaza kwani alikuwa mfanyikazi wa mjengo na alianza kama mchezo kabla ya kuwa muigizaji katika show ya Churchill.

Kulingana na Bernard, kazi za mjengo alianza baada ya kumaliza kidato cha nne, kazi ambayo aliifanya kwa miaka miwili au mitatu. Anasema kazi ile haikuwa rahisi kwani licha ya kulipwa mia nne kwa siku, kuipata sio rahisi.

Nilijiamini kama watu wengine na nikasema nitaweza nikang'ang'ana na nikawabamba na nikasema nitaweza. Mimi ni jamaa wa mjengo na tulikuwa kazi ya kuchota mchanga.

Watu hudharau lakini ni ngumu kupata kwani watu hupeana kitambulisho kabla ya kuingia kwa lorry. Nilikuwa nalipwa 400 lakini siku hizi ni 500. Ile kazi nilifanya baada ya kumaliza shule ya upili kwa miaka miwili au mitatu.

Sasa hivi, Bernard ni jina linalojulikana Kenya nzima kwa ucheshi wake na anafurahia kuwa sasa ametoka kuwa kijana wa mjengo hadi kuwa msanii anayepiga shoo na magwiji kama Eric Omondi, Churchill na MC Jessy.

Anasema kuwa ana furaha kuwa wazazi wake wanafurahia anachofanya akidai kuwa kijijini mamake amekuwa mashuhuri kuliko zamani.

Watu wa kijiji chetu kaunti ya Siaya walinunua TV ili wanitazame na wazazi wangu walifurahia sana kwani mamangu sahii yeye ni mashuhuri. Siku hizi hawezi omba chumvi anyimwe.

Je amejifunza lipi kutokana na hilo?

Nimekuja kujua kuwa lolote lawezekana ukijiamini kwani sikuwahi jua kama nitawahi piga show na Churchill, Eric Omondi na pia MC Jessy na pia kuwa na heshimu na nidhamu.