Matatizo yake yalianzia katika hospitali moja hapa Nairobi ambapo mwanawe alikosa kuhudumiwa na madaktari kwa wakati na kuaga dunia . kwa sababu alikuwa ametumia pesa nyingi kwa matibabu ya mtoto hakuwa na pesa za kutosha kutafuta jeneza na kufanikisha usafiri wa mwili wake kutoka jijini hadi Kwale . Chiti alijaribu kutafuta usaidizi kutoka kwa jamaa na rafiki zake lakini kiasi cha fedha zilizokusanywa hakikutosha kuweza kuusafirisha mwili wa mwanawe .Ni katika hali hiyo alipoamua kwamba liwe liwalo kwani alipanga kuubeba mwili wa mtoto wake katika mfuko wake wa mkononi kutoka Nairobi hadi kwale .
Aliuchukua mwili ule hospitalini na kuuweka katika karatasi na kisha akaukunja katika leso na kutumbukiza kwenye begi lake .Hakuna aliyeweza kujua amebeba nini lakini moyoni mwake alihuzunika sana kuona kwamba hali ya uchochole ilikuwa ikimlazimu kuusafirisha mwili wa mtoto wake kwa njia ile.
Alifika katika kituo cha mabasi ya kwenda Mombasa mwendo wa saa moja jioni na gari lile likaondoka . Akiwa safarini Chiti alikuwa akibubujikwa machozi abiria wenzake wasijue nini kulikuwa kikimliza na waliotaka kujua zaidi aliwaambia alikuwa mgonjwa na hivyo basi maumivu yalikuwa yamemzidi . Begi yake iliyokuwa na mwili wa mtoto wake iliwekwa ndani ya gari katika vyuma vilivyokuwa juu ya kiti chake .Alikumbuka jinsi mlinzi lkwenye mlango wa gari alipomuuliza amebeba nini alimuambia kwamba alikuwa amebeba nguo zake .
‘Nilihofia kwamba iwapo angeamua kuikagua ile begi basi angeupata mwili wa mtoto wangu,ingekuwa kesi kwa sababu hakuna angeyeweza kuamini kwamba nimeshindwa kupata pesa za kuusafirisha mwili huo’ anasema Chiti .
Alipofika Mombasa , Chiti hakuwa na muda wa kupumzika na safari ya kwenda Kwale ikaanza .Alichukua gari jingine hadi kwale huku jamaa zake wakimgonja kwa maazishi .Hawakujua kwamba mwili wa mtoto ulikuwa ukisasafrishwa katika mkoba wa mkoni na wengi walishangaa walipomuona Chiti akiingia bomani bila jeneza wala msafara wa magari . Alipoingia chumbani aliutoa ule mwili ambao sasa ulikuwa umeathiriwa na joto baada ya safari ndefu iliyoanza siku iliyotangulia . Baada ya maazishi Chiti hakuweza kupata nguvu za kuja Nairobi kwa sababu wiki mbili zilizopita kabla ya mwanawe kuaga dunia zilikuwa ndefu kwake .Kifo cha mtoto wake kwa sababu ya utepetevu wa madaktari pia kilimpa kumbukumbu ambazo alitaka saba kuzifuta akilini mwake .