Nilifikiri mmeokoka! Dr Ofweneke awaambia Size 8 na DJ Mo

Siku ya wapendanao msanii Size 8 na mumewe DJ Mo waliweka sherehe ya kupigiwa mfano na wengi, ni sherehe ambayo ilipokea wakosoaji wengi katika mitandao ya kijamii.

Sherehe hiyo ilikuwa katika eneo la Kileleshwa na kuhudhuriwa na watu na wapenzi wengi.

Kupitia kwa picha zilizokuwa katika mtandao wa kijamii, zilionyesha walioalikwa walikuwa na wakati mzuri na mwema, walijivinjari, walikula na hata kunywa vinywaji usiku wote.

Si hayo tu wenye sherehe Size 8 na DJ Mo walionekana wakicheza vyema na kuwa na wakati mwema zaidi usiku huo.

Kadri saa na sekunde zilipozidi kuona ndipo mapenzi yalikuwa yananoga,baada ya mcheza santuri kama DJ Mo alipoingia jukwaani,alikarbishwa na mkewe kwa wimbo uliomfanya Mo kubaki kwa mshangao jinsi binti huyo ambaye ni mkewe alivyokuwa ananengua kiuno.

Wakati Dj Mo alipokuwa akiangalia vile kiuno kilikuwa kinatingishwa ,paparasi nao hawakubaki nyuma kwani waliibui hisia mseto mitandaoni kama njia ya kutoa maoni yao.

Dr Ofweneke akiwa mmoja wao aliandika kwa lugha ya kimombo na kuwauliza swali"I thought you guys were saved" huku akitabasamu.

Hisia mbalimbali zilitolewa, huku wengine wakimwambia DJ Mo alikuwa kwa laini yake, na alikuwa mahali palipokuwa panafaa.

officialkaravillage Head to toe @officialkaravillage. You killed it.

dianah_chacha Kabisa ! 😂😂🔥🔥🔥

vickynyams Enjoy and have fun.. Watu wengi watakuja regret saana..kujifungia juu ya eti oh this oh that. Lol we are here to have fun, live life and make the best of it while you still have your breath.. You guys are a very beautiful couple…

djeuphorique Hahahaha 😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 sijawai ona ukiwa happy vile uko hapo kaka

officialkaravillage The look is epic

muthoka_1 😂😂😂😂😂three course meal na gathufu pia

laura_waswala Mboga yako hii

mcpricekenya Hizi ni zle siku za funkie ukiangukia dame wa shule noma😂😂😂 maboys lazima wakubali.. @size8reborn