massawe-ilikuaje-300x200

‘Nilifungwa miaka kumi kwa kupachika mtoto mimba,’ Jamaa afichua

Jamaa mmoja alifunguka mwanzo hadi mwisho jinsi alivyojipata taabani na kupelekea yeye kufungwa jela kwa miaka kumi.

Kulingana naye, kosa kuu lilikuwa kuvunja sheria na kushiriki ngono na mtoto mwenye umri wa miaka kumi na sita. Na kama hilo halikutosha, jamaa alimpachika mwana wa wenyewe mimba na kuharibu maisha yake.

Mzee wa miaka 67, adaiwa kumbaka mtoto wa miaka kumi na miwili

Akizungumza katika kipindi cha Bustani la Massawe kupitia kwa njia ya simu, alimweleza Massawe jinsi maisha ya gerezani yalivyokuwa magumu kwa kipindi hicho.

Alisema kuwa alipata tabu kula, kulala pia ilikuwa changamoto kwani kunguno walimvamia usiku kucha. Lakini baada ya kutumikia kifungo chake, jamaa alijifunza kazi ya ufundi wa mbao.

Sasa hivi ana duka lake na amemuoa kidosho mwenye miaka 20 na wawili hao wanatarajia kujaliwa mtoto hivi karibuni.

Soma usimulizi wake,

Furaha kwa Kenya? Salah huenda akakosa mechi dhidi ya Harambee Stars

Nilipachika msichana mimba nikiwa na miaka 16 na nikashikwa na kufungwa jela. Nilipotoka sikudhani watanipea mtoto lakini walinipa na msichana yule akarudi shuleni.

Nilikuwa na miaka 19 wakati ule na msichana alikuwa na miaka kumi na sita, na nilifungwa jela kwa miaka kumi. Sahii nikiona mtoto wa wenyewe siwezi mkaribia.

Maisha mle jela yalikuwa magumu kwani kula ngumu, kulala kulikuwa na chawa lakini nilienda Naivasha nikajifunza ufunfi wa mbao na sahii nimefungua duka langu.

Nimeoa mke wa miaka ishirini na sasa hivi ni mja mzito.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments