Msanii huyo wa kibao kilichotambaa cha Golddigger ametoa wimbo mpya kwa ushirikiano na mkenya Arrow Bwoy kwa jina ‘ The One’.
Picha zake akiwa amechanika na huku akikosa kujielewa ziliibuka katika vyombo vya habari nchini mwake na kutokea ripti kwamba alikuwa akitumia dawa za kulevya kama vile cocaine na heroine lakini staa huyo wa zamani wa kundi la Blu 3 sasa ameamua kujitosa tena katika fani ya muziki .
Amezungumza na mpasho kupitia instagram Live na amekanusha kuwahi kutumia dawa za kulevya
Nilikuwa mraibu wa kuituia dawa kwa jina PETHIDINE; ilikuwa dawa ya kupunguza maumivu wala sio dawa ya kulevya na nilianza kuitumia baada ya kupata jeraha la mgongo na nilifaa kufanyiwa upasuaji ila ilikuwa ni jambo la 50-50 uwezekano wa kupoteza maisha yangu au kupona
Alifikiria kuhusu upasuji huo lakini akapatwa na hofu kwamba hangeweza kutembea
(PETHIDINE) ilikuwa dawa ya kunipa afueni ya maumivu haraka na kuanzia mwanzo nilionywa kwamba ningejipata nimekuwa mraibu wa kuitumia ,baadaye nilijipata katika tatizo la kuacha kuitumia dawa hiyo wala sikuitumia kulewa ama kwa raha ni kwa sababu nilikuwa naitumia kupunguza maumivu
Hatua hiyo iliathiri taaluma yake katika muziki na hata akasahaulika .Hakuwa tena akifanya muziki .
“ utumizi wa dawa hiyo uliathiri taaluma yangu katika muziki na ikafika wakati sikutaka kufanya kazi au kwenda studio nilitaka tu kuwa pekee yangu yalikuwa mambo mengine yaliyojichanganya na nikaanza kupata na mawazo kupindukia na wakati watu walipoanza kusema mambo ya kutunga kunihusu niliamua kujifunga kabisa
https://www.youtube.com/watch?time_continue=22&v=foQ5h799PpM&feature=emb_logo
Aliendelea kusema
nafikiri ni jambo zuri lililofanyika kwa sababu singekuwa mwanamke ambaye sasa niko hapa hatua hiyo ilinipa nguvu na kunifunz akwamba watu wanaweza kukuinua na pia wakati mwinginme wanaweza kukukanyaga
Alipoangazia sana ,Chandiru alijipata katika matatizo mengi hasa baada ya mdai kwamba anatumia dawa za kulevya na alijaribu kujiua .
… ndio nilijaribu ,sitakanusha hilo nilitaka kujiua nilikuwa nimechoshwa na kila kitu na hasa habari za wongo katika vyombo vya habari .kulikuwa na ripoti nyingi kwamba nilikuwa natumia dawa za kulevya ilhali hata sijui cocaine au heroin zinafanana vipi