Rappa Khaligraph Jones alizungumzia jambo hilo na kusema kuwa alibaguliwa na mhindi alipokuwa anaenda kununua jumba aliloliona kwenye mitandao ya kijamii.
Khaligraph hakuweza kuingia katika jumba hilo lililokuwa eneo la Lang'ata, kwa maana alikuwa mwafrika.
Rappa huyo aliwauliza watu kwenye mitandao wazingatie jambo hilo ambalo linatendeka humu nchini huku akisema kuwa kuna baadhi ya wananchi ambao wanakubali watu wa rangi au kabila lao kupanga nyumba.
Hasa msanii huyo alizungumzia maeneo ya Lang'ata na Westlands. Swali ni je, ubaguzi wa rangi utazidi kutekelezwa hadi lini na ni lini utakwisha swali ambalo wengi wanaulizana na wanazidi kuulizana.
Alieleza jinsi alifanyiwa wakati huo,
"Mwaka jana nilienda maeneo ya Lang'ata kuona nyumba nzuri ambayo niliona mitandaoni, baada ya kufika huko tulikatazwa kuingia katika nyumba hiyoSababu ilikuwa hawakuwa wahindi ilhali walikuwa waafrika, tuliambiwa tu wahindi pekee ndio walikubaliwa kupangisha majumba hayo
Nilijua ni mazishi nilirudi Kayole polepole, sikupewa heshima."Alieleza Khaligraph.
Baadhi ya wasanii ambao walizungumzia jambo hilo ni kama,