Nilikuwa msagaji nikiwa katika shule ya rehab kwa sababu ya kutumia dawa za kulevya-mwanamke Asimulia

wasagaji
wasagaji
Watu au watoto wengi hupelekwa katika shule za kurekebisha tabia yaani rehab kwa sababu ya vitendo vyao vibaya na kuwasumbua wazazi wao sana.

Lakini kwa mwanamke huyu mambo yalikuwa tofauti baada ya kupelekwa katika shule ta rehab kwa ajili ya dawa za kulevya.

Alieleza jinsi alivyokuwa msagaji alipokuwa katika shule hiyo, baada ya familia yake kuchukua uamuzi kuwa anapaswa kuenda katika shule hiyo.

Kupitia kipindi katika radio jambo, Rose alitoboa siri na kusema,

"Nikiwa katika kidato cha tatu nilikuwa navuta bhangi sana, mama yangu mzazi hakujua chochote lakini ilifika mahali akajua.

Hii ni baada ya wazazi wa marafiki zangu kuniripoti kwa mama yangu, nilitumwa katika shule ya rehab ili nibadilike kwa muda wa miezi tano." Rose Alisimulia.

Rose aliendelea na kueleza vile aligundua anapenda wanawake sana kuliko vile alivyokuwa anapenda wanaume kabla ya kujiunga na shule hiyo.

"Nilianza kuwa na hisia za kimapenzi kwa wanawake, kuna pia mwanamke ambaye alikuwa ni msagaji na tulipendana sana na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi.

Nilimuacha katika rehab, lakini baada ya wiki moja nilipatana na mwanamke mwingie lakini alikuwa anataka tupatane na wazazi wangu.

Baba yangu aliaga dunia ilhali mama yangu hajui kuwa mimi ni msagaji." Rose Alisema.

Rose alisema jinsi amechoshwa na mama yake kwa kumtafutia wachumba ilhali hana haja na wao.

"Mpenzi wangu amenijulisha kwa wazazi wake, nina miaka,21, anataka kunichumbia na atafanya hivyo baada ya kujua na kupatana na wazi wangu

Katika upande huu mwingine mama yangu amejaribu kunitafutia wachumba ambao anafanya kazi na wao, na nimechoka." Alisema Rose.