unnamed.1

Nilikuwa naenda klabu kuskiza mziki tu; Asema mchungaji Burale

Mhubiri Robert Burale amejitokeza hadharani na kusema kuwa licha ya kuwa alipenda sana kwenda kujivinjari kwenye vilabu vya usiku, hakuwahi kunywa pombe maishani mwake kama inavyodhaniwa.

Burale anasema kuwa yeye ni mpenzi wa muziki aina ya Lingala na kila wakati aliskia hapo ngoma yoyote yeye angejirusha ugani kusakata densi.”Niliacha kwenda vilabu mwaka wa 2008 na hata kabla ya hapo sikuwa nimewahi kulewa mbeleni. Nilikuwa naenda kusikiliza muziki kabla ya Mungu kuniokoa.”

Wachezaji waliopatikana na hatia ya ubakaji kuzuiliwa kwa wiki moja zaidi

Burale anasema kuwa angetembelea vilabu mara kwa mara kwa ajili ya kufurahisha macho yake hasa kwenye vilabu vya wanawake (strippers).
Hata hivyo, Burale ameamua kuwapa wanaume wengine ushauri mdogo huku akiwaambia wafanye mambo ya maana badala ya kwenda vilabu kama hivyo.

“Fikiria ukisakata mziki na mtu wa rika ya babako ukienda kushoto, kitambi chake kinakufuata. Kama wewe ni mwanaume wa aina hio basi badilisha tabia zako na ufanye jambo la maana.

Waweza hata kufanya jambo la maana kama kwenda kutembelea wagonjwa hospitalini.”

SOMA MENGI HAPA

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments