black-woman-crying-

Nilimfumania mume wangu na cousin yake kitandani mwetu! – Anita

Wiki hii mtangazaji bi Massawe aliwapa wanawake fursa murwa wafunguke na watoe yaliyo mioyoni mwao kuhus jinsi waume zao waliwacheza kwa kushiriki ngono na jamii zao.
Baadhi ya wengi walijitokeza na kufichua siri ambazo zimefichika miaka na mikaka na hata kama wengi hawakutaka kufichua majina yao, mwanadada mmoja kwa jina Anita hakujali.
Kulingana na Anita kutoka maeneo ya Uthiru, mumewe alimcheza na cousin yake bila aibu!
Akielezea, Anita alisema kuwa siku moja aliporudi nyumbani kutoka kazini, alimfumania mumewe akiwa kitandani na cousin yake. Licha ya kupatikana, mumewe hakujali na Anita alipotaka kujua ni kipi kilikuwa kinaendelea, walizozana na ikageuka kuwa vita.
Hapo ndipo aliamua yameisha na kufunganya virago vyake na kuondoka kwani alijua siku zake kwa ndoa ile zimetamatika.
Aliongeza akisema kuwa aliyekuwa mumewe hujaribu kumpigia simu na kumrai warudiane lakini tendo lile bado humuuma na hakuna jinsi anaweza rudi kwa ile ndoa.
Pata usimulizi wake hapa,

Jinsi ya kuepuka kutongozwa kwenye maeneo ya burudani

Mimi nimewahi pitia hayo mambo! Bwanangu alienda na cousin yake kwani nikienda kazini nilikuwa nawapata wako pamoja.
Siku moja nikawapata kwa bed, kumuuliza ikiwa ni vita so ningefanya nini? Ilibidi niwaondokee.
Hadi wa leo yeye hujaribu kunitafuta lakini hayo machungu bado ninayo.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments