Nilimpoteza rafiki yangu Ayeiya siku ya kulipa mahari yangu - Terrence

Terrence Kamami amefichua vile kifo cha mcheshi wa kipindi cha Churchill Emmanuel Makori almaarufu Ayeiya kilimshtua kutokana kwamba kilitokea wakati ambao alikuwa ameenda kulipa mahari kwa mke wake (ruracio).

Mcheshi Emmanuel Makori Nyambane aliye fahamika kama Ayeiya alikufa baada ya gari lake kugonga mti katika chuo kikuu cha Catholic Eastern Africa barabara kuu ya Magadi.

Aliweza kuongea maneno hayo kwa maana hakuwa na matumaini ya kuishi na alikuwa amechanganyikiwa, aliweza kukumbuka vile alikuwa karibu kubakwa katika eneo la Eastleigh.

Ndugu yake pia alikuwa katika mitaa ambaye aliweza kusaidiwa, na kisha kueleza juu ya Terrence hivyo ndivyo muli alivyo okoa maisha yake.

"Nilienda shule ya msingi ya Saint Bridget kama 'chokora'ambapo niliweza kupata alama 201 juu ya 700, hii inamaanisha nilikuwa naenda shule kisha baada ya shule naenda kutafuta pesa ili niweze kupata chakula,

"Tulikuwa tunangoja hoteli zifungwe ili tuwaoshee vyombo ndiposa watupe chakula," Alisema Kamami.

Katika shule ya watoto mayatima ya Muli, Terrence aliweza kuenda shule ya ukarabati kwa miaka mitatu kisha kurudi shule katika darasa la tatu.