Nilimvunja ubikira na kumuacha mataani,'wanawake wa Afrika Kusini wasimulia dhulma dhidi ya waume

Mtandao wa kuwaalika wanawake kusimulia mambo waliotendea wapenzi wao wa kitambo umepata umaarufu sana wanawake wengi wakifichua siri zao.

Kupitia mtandao wa kijamii wa twitter mwanaume mmoja kutoka Afrika Kusini aliuliza wanawake nini walichokifanya na hawawezi kusahau?  haya hapa majibu yao;

Mmoja alijitokeza na kusema,

"Mpenzi wangu alinipenda na kuniambia kuwa anataka mtoto, nilimdanganya nina mimba alifurahi baada ya siku mbili nilimuambia kuwa nitaavya mimba yenyewe

Ala!! kumbe kunawanaume wanakubali majukumu siku hizi/ si hayo tu mwingine aliandika

"Kuna mwanaume alikuwa ananitaka sana siku moja alinitumia nauli niende kumsalimia kufika huko nilianza kuchumbia ndugu yake." Alisema.

La haula, duniani kuna mambo.

Mmoja wao aliandika kuwa mpenzi wake alikuwa na mpango wa kando alipojua aliharibu gari lake la BMW, mwanamume huyo alimpeleka polisi.  Kisha mwanamke huyo akamwambia aondowe kesi hiyo ili warudiane. Baada ya mwanamume huyo huondoa kesi mrembo alipotea asionekane tena na mwanamume huyo.

"Tulichumbiana kwa miaka miwili nikamvunja ubikira wake na kisha nikamuacha nikaanza kuchumbia mwanamume mwingine.

Nilimwambia ajipange mimi si mwanamke wake." Alisema mmoja wa wanawake.

Si hayo tu haya masaibu mengine;

'Nilikuwa nimekaa na rafiki ya mpenzi wangu akaniuliza nimepanga kumpa 'nunu' lini nami nikamuuliza amepanga kutairiwa lini'

Hawakufua dafu mbali walizidi na mazungumzo yao na siri nyingi zikafichuliwa;

Kwa kweli boy child amepitia mengi ambayo hawawezi simulia na hata kusema mbele ya marafiki zao, je umepitia nini ama ni jambo lipi girl child amekufanyia huwezi ata sahau?