pastor.omba

‘Nilimwaga machozi lakini Gloria Muliro hakunirudia,’ – Pastor Omba

Leo kwenye kitengo cha Ilikuaje, Massawe Japanni alikuwa mwenyeji wake Pastor Omba ambaye ndiye aliyekuwa mumewe msanii mashuhuri, Gloria Muliro.

Omba ambaye ni mchungaji na pia producer, alifunguka mwanzo mwisho kuhusu ndoa yao ambayo ilivunjika miaka kadhaa iliyopita baada ya kuchumbiana kwa mda wa miezi sita pekee.

Je ni ukweli mume wake Gloria Muliro alikuwa na mpango wa kando?

Je ni kipi kilipelekea wawili hao kutengana?

Imepita karibu miaka mitatu minne hivi na kwangu mimi sikupenda kumtenga kwani nilimuoa nikiwa na malengo ya kumuoa milele lakini tukajipata tumetengana.

Omba alikana madai kwenye vyombo vya habari kuwa hakuwa anampiga Muliro haswa ikizingatiwa yeye ni mwokovu na anajua jinsi ya kutatua shida zao.

gloria-muliro (1) (1)

 Mambo ya kusema kuwa nilimchapa kwa sababu hapati mtoto, mtoto anatoka kwa mungu na sisi hatuoani kwa sababu ya watoto ila ni kwa ajili ya mapenzi.

Mimi nilijipata hapa na nikanyamaza na sikumpigia simu kwani alini block kila mahali.

Mhubiri huyu alipoulizwa chanzo chao kutengana alisema kuwa hadi wa leo hajui mbona waliwachana kwani ndoa yao ilikuwa na mambo ya kawaida kama zile zingine.

Dear single, godly men, if Gloria Muliro has been your fantasy, she is free

Isitoshe anasema kuwa alijaribu kumfuata Muliro kufuatia askofu na hata familia na mmoja wao ni askofu Kitonga aliyewaketisha chini ili kusuluhisha shida zao.

 

Walijaribu kila juhudi na sitasahau askofu mmoja alisema ‘siwezi kubali Gloria arudiane na huyu kwani anaweza mkatakata kisha apotelee Congo’. Gloria Muliro naye alisema kuwa mda wake nami umetimia.

Hapo alianza kutoa machozi akidhani atasamehewa lakini wapi! Aliongeza kuwa ilikuwa ni mpango wa mungu kwani huwezi kuamilia au jilazimisha kwa mtu.

 

Photo Credits: Amon mwanjala

Read More:

Comments

comments