Mungu hawachi mja wake, na Mungu ni Mungu wa maajabu atendalo Mola hamna binadamu yeyote atakaye tenda, katibu mkuu wa chama cha Jubilee Raphael Tuju anayajua haya kwa kweli.
Hii ni baada ya kunusurika ajali mbili mbaya moja akiwa katika ndege iliowauwa watu kadhaa
Ajali ya pili ambayo Tuju alikumbana nayo alipokuwa akienda kuhudhuria mazishi ya hayati rais mutaafu Dainiel Arap Moi mwezi jana.
Akiwa katika mahojiano na gazeti la the Star mwanasisa huyo alisimulia jinsi alinusurika ajali ya ndege miaka 17 iliyopita, waliokuwa katika ndege hiyo akiwemo aliyekuwa waziri wa Leba Mohammed Khalif na rubani wawili waliangamia.
"I SURVIVED A PLANE CRASH BEFORE BUT THIS WAS MORE DIFFICULT. I HAD MORE INJURIES THAN IN THE PLANE CRASH." Alieleza Tuju.
Wanasiasa wengine walionusurika katika ajali hiyo ni Martha Karua na Linah Jebuu Kilimo.
.