Buriani Kasee,Ujumbe wa mwisho wa mcheshi Kasee

Kifo cha mcheshi wa churchill show Kasee kiliwaacha wengi na maswali mengi kuliko majibu, hii ni baada ya kupatikana ameaga dunia kwa barabara.

Mengi hayakufahamika kuhusu mcheshi huyo, wengi walimjua kwenye mitandao ya kijamii, kupitia posti yake moja kabla ya kukumbana na mauti, aliandika,

“THE THOUGHT RUNNING THROUGH MY MIND.TRYING TO SECURE THEM BAGS.” Aliandika Kasee.

Kupitia mitandao ya kijamii aliwakashifu wenzake ambao walikuwa wamesema kwamba ana shida ya akili na kuwaambia kuwa,

“MNASEMA KASEE NEEDS MENTAL HELP.. WAJINGA NYINYI #KING KAKA MILELE.”

Katika posti nyingine kasee alisema kuwa amefanya aweezalo humu nchini na yuko sawa nalo, alidokeza kuwa ameonyesha upendo mwingi ilhali hakuupokea kinyume na matarajio yake.

“I SHOWED MORE LOVE THAN I EVER GOT BACK AND IT IS  ALRIGHT WITH ME.”

MHARIRI: DAVIS OJIAMBO