Nilipatana na mume wangu katika mtandao wa kijamii wa instagram-Jackie

Jackie Matubia anafahamika sana katika sekta ya uigizaji kwa muda mrefu sasa huku akipata kazi tofauti katika runinga tofauti.

Akiwa katika mahojiano awali Jackie alieleza jinsi alivyopatana na mume wake, kwa hakika wengi uwa wanapatana katika mikahawa na hata katika hafla tofauti na mbalimbali.

Lakini kwa muigizaji Jackie Matubia ilikuwa tofauti na mahusiano kama yale mengine.

"Nilipatana na mume wangu katika mtandao wa kijamii wa Instagram, nilikuwa na post picha kisha akaanza kuzipenda, kwa mara ya kwanza alipenda picha zangu hamsini

Baada ya hapo alinitumia ujumbe katika mtandao huohuo na uhusiano wetu ukaanzia hapo." Alieleza Jackie.

Jackie aliolewa akiwa na miaka 24 ndoa ambayo haikuduma hata baada ya kupata mtoto wao wa kwanza wa kike ambaye kwa sasa ana miaka mitano.

"Niliingia katika ndoa mapema mume wangu ameniacha na mwaka mmoja, nadhani ndoa yangu ilivunjika kwa sababu hatukuwa tumepewa ushauri na mtu yeyote

Nilienda kumwambia mama yangu kuwa ndoa yangu haikuwa sawa lakini alishtuka sana, ni jambo ambalo lilimadhiri mtoto wangu

Kwa sasa nimepona, kile mtoto wangu anafurahi ni kunioa nikiwa na baba yake, kwa sababu baba yake uwa anakuja kumsalimia na kumuona." Alieleza.

Kwa sasa Jackie anafanya kazi katika runinga ya rembo, kuoneza kuwa iko siku aliyokataa kukonana na marafiki wake  kutokana na mawazo.

"Nilimewakata marafiki wangu wengi kwa maana huwezi amini mtu, si hati ni wao walichangangia ndoa yangu kuvunjika la." Alizungumza.