Nilipiga mpenzi wa mume wangu na alikuwa mja mzito - Joyce

Mwanamke kwa jina Joyce aliwaacha waskizaji wa Radio Jambo vinywa wazi hivi majuzi baada ya kukiri kuwa aliwahi mshambulia mwanamke anaye kisiwa kuwa mpango wa kando wa bwanake.

Kulingana na Joyce, alipewa fununu kuwa kuna mwanamke aliyeonekana na mumewe na kufuatilia alipewa uhondo kuwa yeye huenda kazini mwa bwanake kila mwisho wa mwezi.

Mumewe humpa fedha na isitoshe kumfanyia shopping huku mkewe akiwachwa bila chochote nyumbani.

Joyce hapo aliamua kumtafuta yule mwanamke na kumvamia bila kujali kuwa alikuwa mja mzito.

Soma usimulizi wake,

Naitwa Joyce kutoka Kikuyu na mimi ni mwanaume alikuwa na girlfriend wake wa nje na niliambiwa na rafiki yangu kuwa bwanangu ana mpenzi wa nje.

Mimi sikuwa na haraka, nilienda polepole. Baadaye kuna rafiki yake wanafanya kazi pamoja naye akaja akaniambia kuna mama fulani huenda huko kazini. Ana time siku ya mshahara, pesa ikitokea lazima aitwe anakuja analia shida zake anafanyiwa shopping kila kitu na mimi nimewacha ivyo tu.

Nilitafuta huyo mama nakwambia, nilimtwanga na alikuwa na mimba. Siku yenye alienda na akazaa nilimwambia mwanaume kama anataka kumfuata amfuate.

Sikumhurumia maanake, unajua ukisema kuhurumiana ni wewe utaumia na familia yako. Wamama tunafaa tuangalie, mtu ukijua ana bibi enda polepole wacha kujipeleka mbio mbio.

&feature=youtu.be