Nilipita na mboch juu mke wangu alikuwa analala na trouser (AUDIO)

massawe.000
massawe.000
Jamaa kwa jina Charles alifichua jinsi mkewe alimfanyia masaibu hadi ikambidi alale na mjakazi wao, almaarufu mboch.

Kulingana na Charles, siku moja aliporudi nyumbani kutoka kazini alimpata mkewe akiwa amenuna. Alipofanya juhudi ya kujua chanzo cha hayo mkewe hakuzungumza naye kwa siku tatu.

Katika siku hizo tatu, mkewe alikuwa analala huku akiwa amevalia suruali ndefu na isitoshe alikuwa analala akiwa ameangalia upande wa ukuta.

Jambo hilo lilimkasirisha na hapo akaamua kumtongoza mjakazi wao ili atafute suluhisho la tabia za mkewe.

Akisimulia, Charles alisema kuwa mkewe aligundua na hapo akawaleta wazee wa kanisa nyumbani kwao kutatua shida zao. Hapo walizungumza na tangia siku hiyo tabia zake zilibadilika.

Soma usimulizi wake.

Kuna siku nilikuwa naingia kwa nyumba na mtu amenuna kama mandazi, najaribu kumuongelesha haongei. Haya ikifika wakati wa kupumzika anavaa longi na anaangalia kwa ukuta.

Nikajaribu kama siku tatu mtu haniongeleshi, sasa mimi nikaambia msichana wa kazi kama ni mbaya wacha iwe mbaya ili suluhisho ipatikane. Na suluhisho ilipatikana. 

Nililala na msichana wa kazi vizuri sana ndani ya nyumba yangu wakati mke wangu alikuwa ameenda job na watoto walikuwa shuleni.

Kanisa ikaja kwa nyumba na nikauliza wachungaji analalaje na nguo, shida ni nini? Anavaa nguo kwani anaenda kazini?

Kutoka siku hiyo aliomba msamaha na akasema hatarudia na msichana wa kazi tukamfuta kazi. Siku hizi anavaa suti aliyozaliwa nayo.

&feature=youtu.be