Nilipoteza kazi kwa ajili ya uvutaji sigara-Terence creative asimulia

100859337_2656309174617532_5266499057331897521_n-696x696
100859337_2656309174617532_5266499057331897521_n-696x696
Mcheshi Terence creative almaarufu Kamami, alisimulia jinsi alivyoathiriwa na uvutaji sigari hata kufanya uhusiano wake na mkewe udhoofike kwa muda na hata kupoteza kazi iliyokuwa inampa mkate wa kila siku.

Ni jambo ambalo lilimfanya aache kitendo hicho na kuendelea mbele na maisha. Terence alikuwa anavuta hata pakiti tatu kwa siku moja tu.

"Miaka miwili miezi saba bila kuvuta sigara, nilikuwa navuta pakiti mbili au tatu za sigara kwa siku nilipokuwa kwenye klabu nilivuta shisha pia.

Hata bhangi nilivuta lakini si sana. Marafiki zangu walinifanya niamini kuwa shisha haina madhara mengi kama sigara lakini huo wote ulikuwa ni uongo

Kila uvutaji una madhara na unaweza kuua." Alizungumza Terence.

Mcheshi Terence alisema kuwa madhara hayo yalikuwa mengi hata kutopewa heshima na watu. Haya hapa baadhi ya madhara ambayo alizungumzia;

1. Mke wangu hakuwa ananipa busu kwa hiyo miaka mitano hivi

2.Watu wengi walikuwa wananidharau badala ya kunilipa walikuwa wananinunulia fegi. Huu ndio ulikuwa usemi wao “huyo bora umpelekee fegi, atakujenga “

3.Nilipoteza baadhi ya kazi nyingi kwa ajili ya uvutaji sigara

4.Nilidanganywa kuwa nikivuta sigara nitakuwa mwenye maarifa na ni uongo

5.Nilikuwa natokwa na damu kwenye gamu yangu

6.Kupumua kwa taabu, kuwa na meno yenye chafu na mambo mengine mabaya ambayo yanasababishwa na uvutaji sigara.

Mcheshi huyo aliwahimiza watu na kuwaambia kama yeye alivuta sigara kwa zaidi ya miaka kumi na akaacha si vigumu kwa mtu yeyote kuacha.

Je, wewe unavuta sigara kama mara ngapi kwa siku na ni nini kilifanya uache kuvuta kama ulikuwa wavuta sigara?