allan.muliro

Nilipoteza kazi kwa sababu ya uraibu wa kunywa pombe – Allan Muliro

Allan Muliro, mwigizaji murua wa kipindi cha Inspekta Mwala, akizungumza na vyombo va habari, amedokeza vile ambavyo alipigwa kalamu.

‘Nilipoteza kazi yangu ya upresenta wa show murua ya spoti na burudani viwanjani, na pia uhusiano mzuri na familia yangu ukadidimia kwa sababu ya uraibu wangu wa kunywa pombe.’

Alitueleza pia kuwa, anajuta kupoteza kazi yake kwani baada ya kupigwa kalamu,alipitia makuu, na mara kwa mara anajiuliza maswali. mbona nilijiingiza katika anasa za kunywa pombe?mbona niko peke yangu?’

Alexis Sanchez akiri kuwa hajutii uhamisho wa Man United

Muliro alianza kunywa pombe,mwaka wa elfu mbili kumi na tatu, baada ya mama yake mpwendwa kukata kamba.

”Mimi na mama yangu tulikuwa tumesikizana sana na kifo chake kilinikereketa maini na ndipo nikaanza kunywa pombe hadi mwaka wa elfu mbili kumi na nane nilivyo pelekwa kwenye kituo cha kurekebisha tabia.”

zaidi ya hayo,Allan alitueleza kuwa maisha ya kituo hicho cha kurekebisha tabia hayakuwa mazuri sana.

Hata hivyo, nashukuru kuwa baada ya kuenda kwenye kituo hicho, ameweza kurekebisha ndoa yake na mkewe na kusema pia, apatapo nafasi ya kufanya kazi tena, ataifanya kazi yake vizuri kwani ana uwezo.

Ama kwa hakika, majuto ni mjukuu.

Wabunge watatu watiwa mbaroni wakizuru msitu wa Mau

 Muliro, ambaye ana mtoto mmoja, alimshukuru Abdi Munai kwa kuwa naye, wakati ambapo alikuwa anapitia makuu.

”Namshukuru rafiki yangu wa chanda na pete, Abdi Munai kwa kunipa mawaidha wakati ambao nilikuwa napitia mengi maishani .”

Picha za wanasiasa zinazoonyesha mwonekano wao wa zamani kabla umaarufu

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments