Wema alilazimika kwenda India kwa matibabu kwani iwapo angeendelea kutaka kupata mtoto basi huenda angejipata pia na kansa .
Akizungumza katika mahojiano na Clouds FM Wema amesema ;
‘ sikufanyiwa upasuaji wa kupungu tumbo langu kama wanavyosema watu . sababu yangu kwenda india ilikuwa kupata ushauri na matibabu ya kuweza kupata mimba .
niliporejea nilishauriwa kupunguza uzani kwani hatua hiyo ingezidisha uwezo wangu kumapat mimba kwa sababu ilikuwa na mafuta mengi karibu nza mfuko wa uzazi
Wema ameongeza kwamba baadhi ya tembe alizokuwa akimeza zilikuwa zikimfanya kuzidisha uzani . Tembe hizo pia zilivuruga homoni zake na kufanya kuwa vigumu kwake kupata watoto .
‘ watu wanajua jinsi nilivyojaribu kupata mtoto na furaha yangu itakamilika nitakapopata mtoto .
niliongeza uzani katika jaribio langu la kupata mimba na nimetumia dawa nyingi ambazo zilikuwa na athari za pembeni .