rsz_patience_

Nilipoteza wazazi na mkono wangu katika vita vya 1997 – Patience Dositha

Katika kipindi cha Bustani la Massawe kitngo cha Ilikuaje, mgeni wetu hii leo alikuwa binti kwa jina Patience Dositha ambaye hadithi yake ni ya kuhuzunisha.

Patience ni mzaliwa wa Congo na alizaliwa mwaka wa 1997, mwaka ambao kulikuwa na vita nchini humo, vita ambavyo vilisababisha kifo cha wazazi wake na pia yeye kupoteza mkono mmoja.

Nilizaliwa Congo 1997 na kulikuwa na vita kipindi hicho na aliyenilea alinieleza kuwa wazazi wangu walifarika katika vita hivyo. Nilikuwa na umri wa miezi mitatu na kabla ya babangu kufariki alimshika mama mmoja mguu na kumpa majukumuu ya kunilea.

Anasema wakati huo alikuwa amekatwa mkono na alikuwa anafuja damu sana, na uchungu huo ulimfanya kulia sana. Anasema wauwaji walipokaribia mahala walipokuwa wamejificha, ndipo kilio chake kilizidi.

Hapo wale wauaji waliaamuru wajisalimishe na hapo baba ya familia iliyomchukua alijitolea mhanga na kuwashauri waendelee kukimbia ili wasipoteze maisha yao. Yule mama aliyebaki aliwachiwa watoto watatu huku Patience akiwa wa nne.

Patience anasema kuwa yeye ndiye alikuwa kifunga mimba katika familia hiyo na yule mama mzazi alimpenda kama mwanawe bila ubaguzi. Ila anadai kuwa watoto wenzake hawakuwa wanamuonesha mapenzi kama mmoja wao.

Nikiwa dara la tatu niliulizwa jina la babangu na kuuliza dadangu aliniambia kuwa hajui jina la babangu. Nilipomuuliza mama aliniambia kuwa baba mzazi alienda kwa mwezi.

Aliendelea,

Siku moja tukila miwa nilimwambia dadangu anisaidie kukata na katika ile harakati tulianza kupigana, hilo lilipelekea kuchomana visu.

Anasema kuwa yeye ndiye aliyekuwa mlemavu pekee katika shule yao na alikuwa anahisi kuwa hapendwi kwani hata hakuwahi pata wapenzi shuleni.

Hata baada ya kupitia hayo yote alimaliza shule ya msingi akiwa mwanafunzi bora na hangeweza kujiunga na shule ya upili ya  kwa ajili ya ulemavu. Ilimbidi apelekwe shule ya kibinafsi.

Nikiwa kidato cha tano mama yetu akawa mgonjwa na hatukuwa na fedha za kumpeleka hospitali ya hali ya juu. Siku alipoaga mama alitumana niitwe na tukaomba pamoja huku nikimuahidi atapona.

Nilimuahidi kuwa nataka kufungua kituo cha kuwasaidia watu wenye ulemavu na ambao hawana usaidizi. Ila alikuwa anakaa mnyonge sana na nilishuku kuwa anakaribia kufariki.

Hapo mama alimshika mkono na baada ya kumwomba alale, mamake aliaga dunia. Miaka mitano sasa.

Cha kushangaza ni eti mandugu zake walipoitwa kumuona walimlaumu kuwa yeye ndiye aliyemuua kama jinsi ‘alivyoua baba yao’.

Tangia mama aage aligeuzwa kuwa kijakazi licha ya kuwa mlemavu. Baada ya kuteseka aliamua kurudi Congo ila hakukualishwa kwani hakuwa na hati zinazofaa.

Hapo ndipo alipatana na mzee anayejua, dereva wa masafa marefu ambaye alimsaidia kuvuka boda za nchi kadhaa. Yule mzee alimpa mia tano na ilimbidi awe mtoto wa kurandaranda upande wa Kikuyu.

Akiwa nchini ndipo alipambana na kujipata na shirika lilomsaidia kujiunga na shule ya uanahabari na sasa anafanya kazi za kupiga picha.

Nafurahi kuwa Jeff Koinange ndiye alinichukua kama mtoto wake na hutembea nami na kunipa mawaidha.

 

 

Photo Credits: Ivy Muthoni

Read More:

Comments

comments