Shaffie Weru

‘ Nilitumia mwanamume fare akiwa kamiti nikifikiri ni dame’ Shaffie Weru afunguka kuhusu masaibu

Mtangazaji Shaffie Weru  amesema kwamba wakati mmoja alimtumia   ‘nauli’ mfungwa katika gereza la Kamiti akifikiri kwamba alikuwa akimtumia mwanamke pesa hizo.

Akizungumza na  Kalondu Musyimi wa  Mpasho,  Shaffie amesimulia    masaibu yake akisema;

 ‘ Nimetuma nauli  mara nyingi, saba kabla ya kugundua.

kuna wakati nilituma fare kumbe  NLITUMIA MTU AKO KAMITI ANANYONGA MONKEY.

 Mtu asikudanganye asilimia 99.9 ya wanaume wametuma fare ..sasa nimepata funzo

 Alipoulizwa kuhusu anavyoshughulikia tatizo la wasichana ambao huitisha nauli kila mara Shaffie alisema ;

 ‘Nimejifunza kuwapa blue ticks  na hata wengine nawablock  wakati mwingine unakutana na msichana mzuri na unapomua kumpa ushauri kama huu

‘PESA SIO SHIDA TUMIA YAKO NTAREFUND’  wanakasirika papo hapo

 Wanajibu wakikuambia , ‘SAA HII PESA YAKO KIDOGO NDIO INAFANYA URINGE?

 Unaweza kunusia hasira zao kupitia chats zenu  na kuna wasichana wanaoitisha pesa za  Pizza, salon na vitu vingine

Ameongeza kusema ,

‘Wakati sina kazi nyingi za kufanya au nihitaji  ‘nyama’ freshi  mimi hungia katika DM za wasichana bila huruma

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments