''Niliuzwa kwa wabakaji''Lucia Nekesa afunguka kuhusu maisha yake Iraq

nekesa (1)
nekesa (1)
 Aisee! Mungu hamwachi mja wake.

Mwanamke wa mumu humu Kenya, alifunguka na kusema kuwa alikuwa ameuzwa kwa mbakaji na anashukuru Mungu kwani alimwezesha kurudi nyumbani ambapo ni Kenya, salama.

Lucia Nekesa mwenye umri wa miaka 40, alifikiri kuwa mambo yatakuwa shwari atakapo enda kufanya kazi ng'ambo lakini hali haikua hivyo.

Ilimbidi Lucia avumilie mateso kwa miezi 10 mjini Baghdad nchi ya Iraq.

Akizungumzia kilicho mpata, Lucia alisema kuwa hakuna mtu ambaye anafaa kuenda nchi ya Iraq ama nchi yoyote iliyo maeneo ya kati ya mashariki kufanya kazi za nyumbani.

 “NO ONE SHOULD GO TO IRAQ OR ANY OTHER MIDDLE EAST COUNTRY TO WORK AS A  DOMESTIC WORKER.''Lucy alisema.
Zaidi ya hayo, Lucy alisema kuwa, hawakuwa na maji wala chakula cha kula na mara kwa mara, wangeomba chakula lakini hakuna ambaye angekubali kuwasaidia.
Lucia alisema kuwa, alijipata nchi ya Iraq na alipokuwa akisafiri alikuwa anajua kuwa, anaenda nchini Qatar.
Mama huyu alikuwa anawafanyia kazi watu zaidi ya sita kila siku, na kila wakati aliporudi kwa kaimu wake, (agent) angechapwa sana na kupata majeraha na maumivu tele.

Aliposhindwa kufanya kazi yake vizuri kwa sababu ya majeraha na maumivu, Kaimu wake Rahab na ndugu zake walizidi kumchapa sana na ata kumwita mvivu.
Lucia alikata shauri kuenda kwa polisi kushtaki lakini hakuna chochote kilicho fanywa.
Badala ya kusaidiwa, Lucia aliregeshwa kwa Rahab na Rahab akamuuza kwa jamaa aliyekuwa akimbaka kila siku.
Alipofika kwa bosi mpya, alifikiri kuwa anaenda kufanya kazi pahali pazuri lakini kumbe, alikuwa ameuzwa.
“WHEN I ARRIVED THERE, THERE WERE LIKE 12 OTHER WOMEN THERE. I DID NOT KNOW I WAS SOLD. THEY TOLD ME I WAS GOING TO WORK IN ANOTHER BETTER PLACE. THE WOMEN THERE TOLD ME I HAD BEEN SOLD,” Nekesa alisema.

Miongoni mwa wale wanawake 12 kulikuwa na wawili ambao walikuwa wakenya na pia wao, walikuwa wanabakwa na mwanaume yule.

Zaidi ya hayo, Nekesa alisema kuwa, alikuwa anafanya kazi zote za nyumbani na hakuwa anapewa wakati wa kupumzika labda iwe ameenda kujificha ndiposa alale kwa saa moja peke yake.

“I WAS FORCED TO WORK NON-STOP. I WAS THE CAR WASHER, THE GARDENER, THE SECURITY GUARD, I DID ALL THE DOMESTIC CHORES.

THE ONLY TIME I USED TO REST WAS WHEN I HID FROM MY BOSSES TO TAKE A NAP FOR ABOUT AN HOUR,” Nekesa alisema.

Alipoweza kupiga simu kwenye kundi la haki la binadamu kupitia msaada wa mume wake, wanasheria wa Kenya walianza kufuatilia kilicho mpata Luciana.

Hata hivyo, Rahab alianza kuwaambia watu kuwa alikuwa mwizi na alikuwa na uraibu wa kuwaibia waajiri wake na yeye mwenywe alijua fika kuwa, hakuna mwajiri wake yeyote ambaye alilalamika kuwa Nekesa amemwibia.

Rahab naye alilazimu familia ya Nekesa kutuma shillingi 200,000 ili kufanya mipango ya safari ya kurudi Kenya na yule mwajiri wake mbakaji akaomba shilingi 400 000 ili kumruhusu Lucia asafiri.

Serikali ya Iraqi nayo ilishika doria na kuenda mpaka kwenye ofisi ya mbakaji yule na Lucia pamoja na wale wanawake 13 wakapelekwa kortini.

Wanawake hawa walishtakiwa na makosa mengi jingine likiwa kufanya kazi Iraq bila karatasi halali.

Mabinti hawa walifungwa jela kwa muda wa mwezi mmoja huku wakisubiri karatasi zao za kusafiri ziwe tayari.

Mwishowe, Nekesa alisema kuwa walipokuwa gerezani, alikutana na makahaba, wanawake wasio na akili timamu, waliouza figo zao na watu tofauti tofauti.

Kwa sasa, Lucia Nekesaa ako humu nchini na anashukuru Mungu kwani hajui maisha yake yangekuwa vipi iwapo angebaki kule Iraq.