'Nimefurahishwa na kikosi changu,' Kocha Sebastien Migne

Kocha mkuu wa Harambee Stars Sebastien Migne ametangaza kwamba alifurahishwa na kila mmoja kwenye kambi yake kabla ya kukipunguza kikosi chake hadi wachezaji 23 kwa michuano ya AFCON.

Anthony Akumu, Cliffton Miheso, Brian Mandela aliye na jeraha na Christopher Mbamba ndio wachezaji waliochujwa. Migne amethibitisha kua Joseph Okumu ataanza dhidi ya DR Congo katka mechi ya pili ya kirafiki ya Harambee Stars Juni.

Kenya itaelekea Misri Juni tarehe 19 na itachuana na Algeria, Senegal na Tanzania.

Kwingineko, shirikisho la kadanda nchini, FKF, imetangaza tarehe za mchuano wa kuamua atakayeshushwa daraja lati ya Posta Rangers na Nairobi Stima.

Stima watakua mwenyeji wa mchuano wa kwanza jumamosi tarehe 15 katika uwanja wa Karuturi, Naivasha, huku mkondo wa pili ukichezwa katika uwanja wa Kenyatta mjini Machakos siku tatu baadae.

Mshindi wa jumla atacheza kipute cha ligi ya SportPesa msimu ujao na atakayepoteza atacheza ligi ya NSL.

Tukiangazia Uropa. mkurugenzi mtendaji wa Atletico Madrid Miguel Angel Gil Marin amethibitisha kuwa mshambuliaji wa Ufaransa Antoine Griezmann, mwenye umri wa miaka 28, atahamia Barcelona msimu huu.

Kwingineko Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amepuuzilia mbali madai kuwa anaangalia uwezekano wa kwenda mapumzikoni mwishoni mwa msimu ujao.