'Nimeishiwa nguvu kwa kupoteza chanzo cha kipekee cha kunitia nguvu.'- Mamake Walibora azungumza

83adac509c432871
83adac509c432871
Mnamo tarehe, 15/04 mwaka huu wananchi, viongozi jamaa na hata marafiki  walikumbana na habari za kuhuzunisha baada ya kutangaziwa kifo cha mwanahabari ken Walibora.

Mwili wake ulipatikana katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Kenyatta huku jamaa wakipigiwa simu ili waje watambue mwili huo.

Ken Walibora alitokewa Ijumaa ya pasaka huku nguvu za kumtafuta na kumpigia simu zikiambulia patupu, kulingana na ripoti Walibora aligongwa na matatu kisha kuaga dunia.

Eunice ambaye ni mama wa mwendazake akizungumza alisema kuwa familia na jamaa wamempoteza mtu na mwana wa maana katika maisha yao.

Mama huyo aliyekuwa amejawa na majonzi alisema kuwa Walibora amekuwa wa msaada kwa familia hasa kwa wadogo wake baada y kifo cha baba yake.

“Nimeishiwa nguvu baada ya kupoteza chanzo changu pekee cha kunitia moyo na mtu wa kutegemewa baada ya kifo cha marehemu mume wangu." Eunice Alisema.

Rais Uhuru Kenyatta aliwaongoza marafiki, viongozi na hata jamaa kwa kumuomboleza Gwiji Walibora huku wengi wakimsifia mwenye kupenda elimu na sifa njema.

Kulingana na mmoja wa binamu wa Ken alisema kuwa alikuwa mtu mpole na mwenye kupenda elimu na mengi zaidi.

"Ken alikuwa mtu mpole, angesafiri hadi nyumbani ambapo alijiunga na wazazi wangu siku kadhaa. Alipenda sana mboga za kienyeji, alikuwa akimuomba mama amuandalie akiwa kijijini. Ni jambo ambalo limewaacha wengi na sintofahamu kuhusu mwanamume aliyeishi maisha ya faragha." Alisema.

Ken walibora alikuwa mfano mwema kwa wengi na wengi walipenda kumuiga kwa matendo yake.

Kutoka kwetu wanajambo Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.