Nimempoteza mtu wa maana , aliyekuwa mpenzi wa Papa Dennis asema

Muigizaji wa kipindi cha Machachati Martha Wajero alikuwa miongoni mwa watu ambao alihudhuria ibada ya wafu ya msanii Papa Dennis na kuona mwili wake.

Ibada hiyo iliwekwa ili watu,marafiki,wasanii,wanasiasa,familia wampe Papa heshima ya mwisho kabla ya mazishi yake.

Martha akisoma historia ya mwendazake Dennis alisema maneno haya,

"Nimempoteza mtu wa maana." Martha alinena.

Ni ibada ambayo ilihudhuriwa na wasanii mbalimbali na waliomtaja papa denis kama mtu mnyenyekevu kwa kila jambo alilolitekeleza.

Alitoka muda mfupi baada ya ibada hiyo kukamilika akiwa na rafikiye wa kike.

Baadaye Wajero aliandika katika mtandao wake wa kijamii,

"Within you is the light of a thousand suns 🌠💖." Aliandika Wajero.

Martha na Papa Dennis walikuwa marafiki wa dhati, alipopokea habari kuwa papa Dennis ameaga dunia aliandika ujumbe wake na rambirambi zake kwenye mtandao wa kijamii.

"Mazungumzo ya mwisho ambayo nilizungumza nawe ilikuwa ijumaa saa kumi na moja jioni, kifo chako kilinipa mshtuko mkubwa mpaka sikuweza kuongea kwa muda,

Kwa ajili nilikuwa rafiki yako wa aribu ,Nilikujua kwa muda wa miaka mitano,umekea mwenye kujali,mwenye upendo na mwenye roho njema

Ulipigana na mawazo licha ya yangu kua katika maisha yako,umekua uking’aa kwa njia nyingi ulikua na maisha mema mbele yako kwa maana ulikua mwenye kupenda kazi

Kama vile ulimsifu Mungu kupitia kwa nyimbo zako na kuokoa wengi Mungu ailaze roho yako mahali pema

Umekua pia mwenye kuigwa na wengi, kwa hakika nita kupeza katika maisha haya.” Aliandika Martha.

Kutoka kwetu wanajambo Mungu ailaze roho yake mahali pema.