Nimemsaheme Diamond asema Zari Hassan

Zari Hassan amesema kuwa amemsamehe aliyekuwa mpenziwe, Diamond PLatinumz kwa yale yote aliyomtendea ikiwamo kusema hadharani kuwa Zari alikuwa na uhusiano na Peter wa bendi ya P-Square pamoja na mkufunzi wake wa gym.

"Kuna jambo la umuhimu katika kuwasamehe watu. Mimi nimemsamehe kwa mambo yote aliyonifanyia kwani kwa sasa nipo katika mahali pema kuliko nilivyokuwa mbeleni," Zari alieleza Millad Ayo.

Zari pia amesema kuwa atahakikisha kuwa wanawe Tiffah na Nillan wamemsamehe baba yao kwa kuwaacha peke yao."Kwa sasa wao ni watoto wachanga sana ila singetaka Tiffah awe na kinyongo na baba yake," Zari alisema.

Zari aliweka wazi kuwa alikuwa na matamanio ya kufunga pingu za maisha na mkali huyo wa Kanyaga huku pia akisema kuwa Diamond alikuwa anajua jambo hilo. Hata hivyo, Zari amekanusha madai kwamba alikuwa na uhusiano wa ngono na Peter wa P-square.

Kwenye mahojiano ya hapo awali, Diamond alisema kuwa Zari alipeleka tunda nje ya familia kwake Peter jambo lilokuwa chanzo cha mwisho wa ndoa yao.

Pamoja na hayo ,Zari alisema kuwa picha alizokuwa anazungumzia Diamond alipigwa mwaka 2011 wakati alikuwa na uhusiano na marehemu bwanake, Ivan.

Kwa sasa, Diamond anatoka kimapenzi na binti wa kikenya,Tanasha Donna na ambaye wanatarajia mtoto hivi karibuni.