''Nimerogwa!'' Akiri mwizi baada ya kuiba mafuta ya kujipaka

lotion
lotion

Jamaa mmoja aliyeshtakiwa kwa kuiba mafuta ya kujipaka kwenye duka kuu la Naivas alifunguka na kusema kuwa kilichomsababisha atekeleze wizi ni uchawi.

Edward Macharia mwenye umri wa miaka 70, alisimama mbele ya korti ya Makadara na kukubali mashtaka ya kuiba chupa mbili za mafuta yanayogharimu shilingi 1,720.

Edward aliiba mafuta haya tarehe 20 mwezi wa tisa kwenye duka kuu la Naivas, barabara ya Jogoo.

Macharia ambaye amepewa kiapo cha kufungwa miaka tatu, aliomba msamaha na kusema pia yeye mwenyewe haelewi ni vipi amekuwa akiiba mafuta ya aina moja kwenye duka moja.

“I am very sorry for the offence and I cannot tell why I keep stealing the same kind of lotion from the same supermarket,” Macharia alisema.

Jamaa huyu alikuwa ameshtakiwa kwa kosa lilo hilo mwezi wa nane na hata wakili Merisia Opondo alipomuona, alishtuka na kumuuliza mbona hawezi rudi nyumbani kwani yeye ni mzee.

“At your age, it is shameful to be committing such offences,” alisema.

Macharia naye alikiri atarudi nyumbani iwapo korti itamsamehea hata hivyo, wakili Merisia alikataa na kumwambia wakili mwengine asimamie kesi hiyo.

Ripoti ya kushtakiwa ilisema kuwa, maneja wa duka kuu la Naivas na mkuu wa kamera za CCTV walikuwa kazini walipoona Macharia akiingia kwenye duka lile kama mteja wa kawaida .

Zaidi ya hayo, inasemekana kuwa, alichukua kikapu cha kununua vitu na kuweka mafuta hayo kisha akaenda kununua chumvi ya shilingi kumi.

Macharia aliweka mafuta haya kwenye mfuko wa koti lake na alipokuwa akielekea kutoka, mkuu wa kamera za alipiga kamsa na maneja akakimbia kumkamata.

Baada ya dakika chache, Edward alipelekwa mpaka kwenye kituo cha polisi cha Jogoo.