Nimetoka Market sasa ,niko na Mtu ! asema Cindy Sanyu

NA NICKSON TOSI

Mwanamziki kutoka Uganda Cindy Sanyu hayupo tena kwenye mauzo ya wanawake ambao wanatafuta wachumba wa kuwadekeza sasa,hii ni baada ya mpenzi wake Joel Okuyo Atiku Prynce kuwasilisha ombi la kutaka kumuoa wakati walipokuwa katika mkahawa fulani

Katika video hiyo ambayo Cindy aliituma kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha mwanamume mmoja akiinama chini kwa mguu mmoja na kumuuliza swali iwapo atamuoa na kuwa mpenzi wake wa maisha .

Cindy anaonekana akitokwa na machozi na kukubali kuwa atamuo kisha anampiga pambaja akimsimamisha huku muziki ukidunda chini kwa chini.

Tumebaini kuwa Cindy na mpenzi huyo wake wamekuwa wakionekana kwa muda na sasa wameamua kuweko mambo wazi ili mashabiki wao wafahamu kinachojiri baina yao.

Cindy kwa wakati mmoja alikuwa akifanya kazi chini ya lebo ya Grand Pa ya humu nchini kabla ya mkataba wake kutamatika.

Mpenzi wake Okuyo kwa upande wake ni muigizaji maarufu anayefahamika katika filamu nyingi ikiwemo The Mercy of Jungle,The Bad Mexican,November Tear na nyingine nyingi.