Nina uhusiano na ma pastor wawili na sponsor - Emily

Kama ilivyo desturi, kipindi ukipendacho cha Massawe Japannni, Bustani la Massawe hukuwacha ukiwa mchangamfu, ukiwa umeelimika na isitoshe ukiwa umetosheleza kiu yako ya mziki na burudani.

Siku kadhaa zilizopita ilikuwa zamu yake mwanamke mmoja kwa jina Emily, kuwaacha waskizaji vinywa wazi. Hii ni baada yake kusimulia kuwa licha ya kuwa ameolewa, tatizo lake la kutopata mtoto lilimskuma kutafuta uhusiano nje ya ndoa.

Jitihada zake zilimfikisha kwa pastor mmoja ambaye baada ya uhusiano alimpachika mimba.

Isitoshe Emily hakuwachia hapo kwani alishikana na pastor mwingine kama mpango wa kando, kabla ya kuangukia jibaba kama sponsor.

Anasema pastor yule aliyempachika mimba sasa hivi hayuko kwa ndoa yake na alichobakia ni kumuahidi Emily kuwa atamuoa, na sasa anangojea aone jinsi mambo yatakavyokuwa.

Soma usimulizi wake,

Niliolewa na mume wangu sasa nilikuwa nimetoa mimba na nikakaa bila kupata mimba na akaanza kunisumbua kuwa siwezi pata. Nikaangukia pastor nikalala na pastor akanipa uja uzito.

Sasa hivi nina sponsor na pastor mwingine. Pastor huyu aliwachana na nyumba yake na aliniahidi atanioa lakini tutaona tu.

&t=4s