Nipe Nikupe:Maseneta walimana makonde baada ya ushindi wa Ole Kina

Maseneta wawili wateule - Beatrice Kwamboka  na  Mary Seneta  walipigana makonde  bungeni  wakati wa uchaguzi wa naibu mwenyekiti  wa kamati ya bunge kuhusu afya .

Patashika ilizuka muda mfupi baada ya seneta wa Narok  Ledama Ole Kina  kutangazwa mshindi wa kinyang’anyiro hicho  dhidi ya  Seneta.

Seneta  alikuwa akiungwa mkono nan a baadhi ya  wanakamati hiyo wakiongozwa na  naibu kiranja  wa walio wengi  Farhiya Ali.

Kulingana na maseneta waliokuwa katika mkutano huo kundi la  Farhiya lilitumia sahihi bandia ya seneta Millicent Omanga ili kumpa ushindi   Seneta .