'Nitakupokonya Diana na niende naye marekani.' Aliyekuwa mumewe Eunice Njeri amtishia Bahati

Kwa siku kadhaa sasa msanii Bahati na mkewe Diana Marua wamekuwa wakienea sana kwenye mitandao ya kijamii kwa kukejeliwa na mashabiki wao.

Wasanii wengi na mashabiki walimtetea na hata wengine kumkejeli licha ya kuwa ni msanii mwenzao.

Aliyekuwa mume wa mwimbaji Eunice Njeri, Isaac Bukasa almaarufu rapa Izzo amemuomba msanii wa nyimbo za injili Bahati kujirekebisha ama atampokonya mke wake.

Rapa huyo alimuonya Bahati kuwa huenda akamchukua Diana Marua kwa sababu anahitaji mwanamume ambaye amekomaa kiakili.

Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Izzo alikuwa na ujumbe huu wa kumwambia Bahati, baada ya kuposti picha ya mkewe Bahati.

" if you wont style up, I will fly in Diana and give her a better Life in the USA, she needs a better mature man not just forced tiny beards with no brains.

Stay warned. You are either fully in God or out completely.

Thank you for your advice on Gospel artists." Aliandika Izzo.

https://www.instagram.com/p/B_ajt4qhfud/

Matamshi yake Izzo yanakuja siku chache baada ya Bahati kuposti video akiwa amevalia vipuli na nguo ya Diana huku akiwa anacheza.

https://www.instagram.com/p/B_aVUJfDeFs/