'Nitamsamehe kwa kuvua nguo iwapo ataomba msamaha,' Jamaa aambia mahakama

mahakama
mahakama
Nitamsamehe kwa kuvua nguo lakini kwanza aniombe msamaha kupitia kuandika barua na aahidi kuwa hatowahi vua nguo tena katika uwanja wa ndege wa Wilson.

Hayo ndio maneno Mkurugenzi wa Chuo cha Aeronautical Kenya, Samson Aketch aliyoambia mahakam Jumanne kama masharti ili aweze kumsamehe mwanamke ambaye alikiri kuwa wanachumbiana.

 Mnamo Julai 3, bi Dorcas Nduku alishtakiwa kwa kuvamia uwanja wa ndege wa Wilson na kusababisha usumbufu baada ya kuvua nguo hadi suruali ya ndani kabla ya kupiga kelele. Inadaiwa kuwa alidai kumuona Aketch.

Nduku hata hivyo alikanusha madai hayo mbele ya hakimu mkuu wa Kibera, Derrick Kuto. Alisema kuwa Aketch alikuwa amemualika amtembelee, akisema walikuwa wamechumbiana kwa mda mrefu.
Aketch alikuwa akituma ujumbe wa mapenzi.

Hati za korti zilionesha kuwa polisi na walinzi walijaribu kumtimua Nduku na hapo ndipo alivua mavazi huku akisalia tu na suruali ya ndani.

Jumanne Nduku alionekana mtulivu na hakusema lolote pindi tu hakimu alipoagiza wawili hao waelewane na kisha waarifu mahakama.

Hakimu mkuu Renee Kitagwa alisema mashtaka hayo yatatolewa iwapo watakubaliana na kusameheana.

Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 28.