Nitapigania "haki yangu," Sarah Wairimu aapa

sarah wairimu (wecompress.com)
sarah wairimu (wecompress.com)
''Tupo hapa kumzika Tob kwa mara ya pili, lakini wakati huu kwa hadhi.'' Haya ni maneno yaliyosemwa na Benard ambaye ni kaka yake Tob Cohen.

Simanzi ilitanda katika hafla ya mazishi ya bwanyenye Tob Cohen, Jumanne alasiri.

Mjane wake Sarah Wairimu alisema kwamba atapigania" haki zake".

Mwili wa Cohen uliondolewa kutoka hifadhi ya maiti ya Chiromo na kupelekwa katika makaburi ya Kiyahudi yaliyopo barabara ya Wangari Maathai.

Baadhi ya watu mashuhuri waliokuwa katika hafla hiyo ya mazishi ni pamoja na Balozi wa Uholanzi, Captain Kung'u Muigai na Ngengi ambao ni binamu zake rais Uhuru Kenyatta.

Baada ya hotuba, ni wayahudi pekee waliokubaliwa kushuhudia kuzikwa kwa Tob katika kaburi lake.

Mazishi ya Tob yaliahirishwa baada ya kukosekana kwa idadi itajika ya makasisi kulingana na desturi za Kiyahudi.

Waliojitokeza Jumatatu walikuwa 8 kati ya 10 waliohitajika ili kutelekeza wajibu huo.

Cohen aliripotiwa kupotea katika nyumbani kwake Lower Kabete kati ya Julai 19 na Julai 20.

Hatimaye mwili wake ulipatikana  majuma 8 baadaye katika tangi ya maji ardhini.

Mwili wake ulikuwa umefungwa na mifuko kadhaa ya plastiki ulipotolewa.