Nitasheherekea birthday miji ya London, Paris, Washington na New York - Gidi

Hii leo kama ulikuwa unaskiza kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi utakumbuka kuwa leo mitambo iliharibika na kusitisha shughli za patanisho, kipindi kipendwacho na mamilioni ya wakenya kote duniani.

Hata hivyo waskizaji walipata fursa ya kupiga simu na kupeana maoni yao kuhusu kitengo hicho huku wakieleza jinsi kimesaidia ndoa nyingi na kubadilisha maisha ya wengi.

Kabla ya show kutamatika, Gidi pia alisema kuwa hatakuwa hewani wiki ijayo kwani mwezi huu mpya ujao wa Septemba, atakuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa.

Gidi alizaliwa miongo kadhaa iliyopita tarehe 5 Septemba, na kila mwaka yeye huhakikisha kuwa amejivinjari vilivyo lakini kitu ambacho hupenda kufanya ni kusafiri hadi Ufaransa kuitembelea familia yake kwa siku kadhaa.

Mwaka uliopita, Gidi alifanya jambo la busara sana kwani alipanga sherehe ambayo aliwaalika marafiki zake na wakuu kutoka nyanja mbali mbali humu nchini.

Sherehe hiyo iliyo andaliwa katika hoteli ya Ole Sereni, Nairobi ilikuwa na nia moja tu; Kuchangisha fedha za kusaidia wagonjwa wa saratani.

Kupitia mtandao wake wa Instagram, Gidi ametangaza kuwa atakuwa anasheherekea birthday yake katika miji minne mikuu duniani.

Gidi ambaye ameanza likizo yake rasmi anapangia kuzuru London (Labda kutizama mechi ya Arsenal), Paris (Ufaransa), Washinton DC (Marekani) na pia New York City.

Ziara yake inaanza tarehe 2 na kukamilika tarehe 10.

Gidi aliandika,

BREAKING NEWS: officially on leave and the birthday boy is on the lose. 4 Cities birthday treat starting tommorow in London, Monday 2nd in Paris, 6th in Washington DC, 10th in NewYork City. Plan accordingly n hola. Work hard play hard. Ciao 👊🙌