Njama A-Z ya kuiba hela Barclays, kisa cha Standard Chartered tofauti mno

barclays
barclays
Makachero wamewanasa washukiwa wa wizi katika benki ya Barclays na kuwatia nguvuni.

Jacob Barasa, Hillary Ng'eno, , Douglas Momanyi na Jared Nyang'au wameripotiwa kupatikana katika jaribio la wizi.

Kisa hiki kilifanyika tarehe 22 Oktoba usiku.

Kwa mujibu wa idara ya upelelezi ya jinai (DCI), washukiwa hawa wanne walikuwa wamejihami kwa mifuko kubwa ya kupakia noti katika ATM ya benki hiyo.

Njama ilikuwa imepangwa ikapangika huku wanne hao wakiwa wamesafiria pikipiki ili kutoka mbio baada ya kutekeleza uovu huo.

https://twitter.com/DCI_Kenya/status/1186927204875194368

Kwa sasa simu na pikipiki za wanne zao zipo katika mikono ya wanapolisi huku uchunguzi ukifanyika kubaini chanzo cha kisa hiki.

Maafisa wanaopeleleza kisa hiki wanahoji kuwa mmoja wa washukiwa hawa alikuwa mhudumu katika kampuni ya ulinzi ya KK Security mtaa wa Runda.

"Tumefanikiwa kunasa simu na pikipiki ambayo walikuwa wakitumia, mfuko ambao wangepakia helai,"Makachero

Visa vya raia kuvamia benki zimekithiri sana nchini.

Ni juzi tu kima cha Milioni 72 kiliibiwa benki ya Standard Chartered.

Katika jaribio hili la wizi, wahusika walionekana kufahamu usafirishaji wa hela hizo kutoka makao makuu ya G4s katika sehemu ya viwanda jijini kuenda benki ya Standard Chartered iliyopo Magharibi mwa mji wa Nairobi.

Hakuna nguvu zilitumika katika wizi huu.

Kesi hii ipo kortini na hatiman yake bado haijajulikana.