Njama ya Ruto na TangaTanga 'kuiteka nyara' Jubilee kutoka kwa Uhuru Kenyatta

Screenshot_from_2019_11_17_14_59_00__1573991972_81129
Screenshot_from_2019_11_17_14_59_00__1573991972_81129

Wandani wa Ruto sasa wanamsukuma 'kuteka nyara' chama cha tawala cha Jubilee kutoka kwa uongozi wa Uhuru Kenyatta.

Haya yanajiri baada ya mkutano wa jamii za GEMA kukutana katika ikulu ndogo ya Sagana kujadili maswala ya BBI na kuziba nyufa zinazofanya wabunge kugawanyika katika vikundi vya TangaTanga na Kieleweke.

Kundi la wabunge wa TangaTanga lipo katika juhudi za kuchukua kiti alichokikalia Uhuru mwaka wa 2022.

Hawa ni wabunge kutoka bonde la ufa na mlima Kenya waliokaidi wito wa rais wa "tuache kampeni tufanye kazi kwanza."

 Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, wengi wa wabunge wanahoji kuwa tukio la Uhuru kuita mkutano wa mlima Kenya wala sio wabunge wote wa chama cha Jubilee ni ishara kuwa hana nia njema na maisha ya usoni ya chama hiki.

Ndoa ya Ruto na Uhuru inaonekana kusambaratika baada ya 'Handshake' iliyofanyika mwaka jana.

Wandani hawa wa Ruto wameapa kuyapuuzilia mbali mapendekezo ya BBI punde tu yatakapochapishwa.

Wachanganuzi wa siasa wanahoji kuwa Ruto anatakiwa ahakikishe hakuna nyufa zozote katika chama hiki iwapo atataka kutwaa ushindi na kuchukua hatamu ya urais mwaka wa 2022.

Katika mkutano uliofanyika bonde la ufa Jumamosi, Ruto aliwaonya waasi wa chama cha Jubilee wanaotapatapa vyama vingine watoke au wajirudi.

Wandani hawa wa Ruto wanapendekeza uchaguzi wa chama ufanyike mwaka ujao 2020 ili kuwachuja 'watu wa rais Uhuru' katika nyadhifa za uongozi.

“Lengo la chama cha Jubilee kwa sasa linafaa kumzuia Raila Odinga kuvunja chama kama jinsi alivyofanyia vyama vilivyotawala. Alivunja KANU, NARC, CORD na sasa anakujia Jubilee." Cherargei alisimulia Daily Nation.

“Ni wazi kuwa Ruto ni yeye pekee anayetaka chama hiki kiwepo na anafaa 'akimbie' nacho" ,Alisema Bwana Chebunet.

Je, Ruto atafanikiwa kufanya jinsi wandani wake wanamshauri?