Njambi wa TRHK afunguka kuhusu mahusiano na mumewe

Screenshot_from_2019_12_12_09_15_52__1576131593_61094
Screenshot_from_2019_12_12_09_15_52__1576131593_61094
Muigizaji wa filamu katika The Real Househelps of Kawangware actress Njeri Gachomba maarufu kama Njambi amefunguka kuhusu mumewe katika video aliyoichapisha katika mtandao wa YouTube.

https://www.instagram.com/p/B5rSboJHp6F/

Haya yanajiri siku chache baada ya kuwashukuru waliompa nguvu na kumuombea katika kipindi kigumu cha kujifungua.

Kupitia mtandao wa Insta, Njambi alisema kuwa aliumwa kwa masaa kumi na mawili.

" Nilikumbwa na maumivu ya leba kwa masaa kumi na mawili lakini nashukuru Mungu malaika wangu aliwasili duniani salama, asante kwa wale wote waliosimama nani, " Njambi aliandika Insta.

 Njambi amesema kuwa yeye na mumewe hawana matatizo na kuwa hawezi kutamani mumuweka wazi ajulikane katika mitandao ya kijamii.

Muigizaji huyu amesema kuwa hangependa kuanika mahusiano yake hivi kuweka usiri mkubwa sana.

Aidha, Njambi alikuwa anachapisha picha za mumewe katika mitandao hapo awali ila kwa sasa anaonekana kuchukua mtazamo tofauti wa kuweka mapenzi yao katika hali ya usiri.