Njia 5 za kuzuia kusota wakati huu wa kwarantini

Ni rahisi sana kufikiria Kuwa nyakati hizi za quarantine zaweza kukusaidia kuweka feha kadhaa kwa akiba ikilinganishwa na wakati ambapo una shughuli kadha wa kadha. 

Lakini hata hivyo, wahitaji uwajibikaji mkuu kukuwezesha kutotumia fedha vibaya.

Kile ambacho wengi hawatokubaliana nami ni kuwa ni rahisi mno kusota wakati huu wa quarantine ukilinganishwa na wakati ambao uko kazini humo nje.

Hata hivyo, nimeunda orodha ya vitu ambavyo vitakuwezesha kuweka fedha nyigi kwa akiba na kukuwezesha kutumia fedha kiasi hadi nyakti hizi za Coronavirus zifike kikomo.

Tumia fedha za usafiri kununua bidhaa vya nyumba

Zimetimia majuma mawili tangia wananchi wngi kuanza kufanyia kazi kutoka manyumbani mwao, na hilo lamaanisha kuwa bado wengi wana fedha ambazo walikuwa wametenga za usafiri.

Pendekezo langu ni kabla hujamaliza hizo fedha unastahili kununua vyakula na bidhaa unavyohitaji vya nyumba.

Zuia kununua bidhaa usivyohitaji

Wakti unaponunua bidhaa unavyohitaji, ni muhimu kujizuia kununua vitu ambavyo havina maana sasa hivi na kuweka umuhimu zaidi kwa vyakula na vitu unavyotumia kila siku.

Kumbuka kununua vyakula vingi ambavyo haviwezi haribika haraka kwa mfano, ndengu, mbaazi na maharagwe.

Punguza fedha za vileo

Watu wengi huwa wametenga kando fedha za vileo na za kujiburudisha mara kwa mara kila mwezi.

Hata hivyo, sasa hivi ni vigumu sana kwa wananchi kujiburudisha katika baa kwa sababu ya kuzuia usambazaji wa coronavirus. 

Badala ya kutegemea baa mbona usinunue vileo vyako katika maduka ya jumla ambapo huwa na bei rahisi ikilinganishwa na baa?

Tumia kadi za supermarket

Mara kwa mara mimi hujaribu kutumia kadi za supermarket ili niweze kujizolea alama ambazo baadaye nitatumia kununua bidhaa wakati ambapo sina fedha zakutosha. Hii pia yaweza kuwa njia nyingine ya kuhakikisha umetumia fedha kiasi zaidi.

Lipa bili zako mapema

Ili kujiepusha kutumia fedha ambazo hujatenga ni muhimu kulipa bili zako mapema kama vile, kodi ya nyumba, bili ya stima, maji na pia  data.