Katika kesi hiyo , Megascope Ltd iliwasilisha kesi kortini kuishtaki NMG na mwanahabari Dennis Okari kwa kuihusisha na sakata katika shirika la Kemsa na hivyo basi kuiharibia jina kampuni hiyo .
Jaji Joseph Sergon jumatano ametoa agizo la kuitaka NMG kuindoa taarifa hiyo mitandaoni baada ya Megascope kuwasilisha ombi hilo hadi kesi hiyo sikizwe na kuamuliwa .
Taarifa hiyo ya upekuzi iliwekwa Youtube na kufikia sasa ilikuwa imetazamwa mara 700,000
Wakili wa megascope Njoroge Regeru alikuwa ametoa ombi kwa jaji akisema taarifa hiyo kuslaia katika mitandao ya kijamii iliendelea kuharibu sifa za kampuni ya mteja wake . Hata hivyo ombi hilo lilipingwa na wakili wa NMG Kiragu Kimani akisema maagizo yaliyotolewa hapo awali kwamba wasiandike taarifa zaidi kuihusu megascope na sakata hiyo yalitosha .
Kesi hiyo itatajwa Oktoba tarehe 22 .