No apologies !Anita Nderu asimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake

Mtangazaji Anita Nderu amesimama kidete na uamuzi wake wa kuwaleta mashoga katika kipindi chake cha upishi Instagram. Akizungumza na Massawe Japanni   katika kipindi chake cha Ilikuaje kwa njia ya simu ,Nderu amesema ingawaje anaheshimu maoni ya watu na misimamo yao kuhusu ushoga ,katu hataomba radhi kwa uamzi wa kuwaleta rafiki zake hao  ambao ni wapenzi wa jinsia moja

https://www.instagram.com/p/CCL3S8Uhom9/

Nderu alizua mhemko mtandaoni baada ya kurushiwa cheche za shutuma  na watu wengi kwa kuwaleta wapenzi wa jinsia moja katika kipindi hicho ambapo walionekana wakipika na kufanya densi densi mtandaoni . baadaye   watu wengi walianza kumtumia jumbe za kumkashifu kwa upotofu wa maadili  wakimtaka aiondoe video hiyo mtandaoni lakini hajatikisika .

Alipoulizwa na Massawe iwapo naye pia ni shoga amesema hilo ni jambo la kibinafsi na atajitokeza endapo itahitajika au  wakati ufaao ingawaje kwa sasa amebainisha wazi kwamba anaunga mkono wa  jamii ya LGBTQ.

https://www.instagram.com/p/CCIEZkBh7RG/?utm_source=ig_embed

Ameongeza kwamba  hatosita kuwaleta tena watu  wa jinsia moja katika makala yajayo ya kipindi chake instagram kwani  kila mtu anafaa kuheshimu maoni ya wengine .

‘Nakataa kuomba msamaha kwa kuwaruhusu rafiki zangu kuwa jinsi walivyo,nakataa kuomba msamaha kwa kupeperuha episode hiyo kwa sababu ni yangu ,ingawaje naheshimu uamuzi wa wale ambao hawajapendezwa na kipindi hicho’