No beef? Ruto alijikaanga mwenyewe asema Atwoli

Katibu mkuu wa muungano wa wafanyikazi nchini COTU Francis Atwoli amesema hana tofauti za kibinafsi na naibu wa rais William Ruto .

Atwoli,  ambaye ni mkosoaji mkubwa wa Ruto amesema wawili hao wanatofautiana tu  kisera na  falsafa za kisiasa .

‘Sina kinyongo na Dp Ruto ,ni mkenya .Na leo anaweza kunialika kwake tule pamoja name pia nifanye hivyo ‘ amesema Atwoli

Kiongozi huyo wa COTU   amejitokeza kama miongoni mwa wanaopinga vikali azma ya Ruto kumrithiri rais Uhuru Kenyatta baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.Ameongeza kwamba Ruto ndiye anayefaa kujilaumu kwa hatua ya washirika wake kupokonywa nyadhifa  za uongozi katika senate .

Wale ambao tayari wamefurushwa kutoka nyadhifa hizo ni pamoja na   seneta wa Elgeyo-Marakwet Kipchumba Murkomen  seneta wa  Tharaka Nithi  Kithure Kindiki  na seneta wa nakuru   Susan Kihika . shoka hilo la kuwaondoa washirika wa Ruto kutoka nafasi za uongozi sasa linaelekezwa bungeni .

Kulingana na Atwoli ,Ruto hajaliwa muaminifu kwa rais Kenyatta na ameendeleza kampeini za kuchukua usukani kabla hata muda wa Kenyatta afisini haujatamatika.

Amesema kuondolewa kwa viongozi wanaomuunga mkono Ruto kutoka nafasi zao hakufai kuchukuliwa kama hila dhidi ya viongozi fulani  au jamii zao .