Tangu alipotengana na msanii wa bongo Diamond, Tanasha amekuwa akiepuka kabisa kufanya hivyo na hata walipokuwa pamoja na nyota huyo, ni familia yake iliyokuwa ikiwek picha za mtoto wa Diamond katika mitandao ya kijamii.
Tanasha hata hivyo aliamua kuitumia siku spesheli ya akina mama kuiweka picha ya mtoto wake huku pia akimshukuru Diamond kwa kumpa kitu kimoja maishani ambacho anakidhamini sana –mtoto wake
Alaindika ;
“My lil big brown eyes growing so fast. Te amo siempre mi amor. I am super proud to be your mother, you make me a better person by the day. I pray to God that you grow up to be positive, humble, successful, kind & most importantly God Fearing. I thank your father for blessing me with you as well… My baby NJ I will always love you & do everything in my power to protect you… HAPPY MOTHERS DAY TO ALL THE BEAUTIFUL MOTHERS IN THE WORLD. ”
Tangu Tanasha aliporejea Kenya, Diamond hajapata muda na mtoto wake lakini pia janga la virusi vya corona limezuia watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine. Wengi wanataraji kwamba wawili hao hawatakuwa na uhusiano wenye machungu kwa minajili ya mtoto wao Naseeb Junior kwani uhusiano mbaya kati ya Zari Hassan na Diamond umevuruga uwezo wao wawili kuwatunza wanao wawili kwa pamoja.