NO PAYRISE: TSC yasitisha nyongeza ya mishahara ya walimu 103,624

Tume ya kuwaajiri walimu TSC  imesitisha  nyongeza ya mishahaya ya walimu  103,624  ambao ni wanachama wa muungano wa KNUT .TSC imesema  nyongeza hiyo ya malipo haikujumuishwa  katika awamu ya tatu  ya mkataba wa CBA   wa 2017-2021  baada ya mahakama kuamua kwamba masharti hayo yategemee  mikataba ya utendakazi na  sio mwongozo wa ustawi wa taaluma za walimu hao  kama ilivyotaka TSC .

TSC imesema kwa sababu ya uamuzi huo  ,haingeweza kutekeleza nyomngeza hiyo ya malipo  chini ya awamu ya tatu ya kutekeleza makubaliano ya CBA . Walimu watakaoathiriwa ni  pamoja na walimu wakuu , manaibu wao na walimu waandamizi . Mzozo kati ya TSC na KNUT kuhusu  mikataba ya utendakazi ,kuajiriwa kwa  mikataba ,uhamisho wa walimu ,kupandishwa vyeo kwa walimu  na ustawi w ataaluma zao  ulifikihswa kortini  baada ya TSC kuushtaki muungano wa KNUT  ili kuzuia mgomo wa walimu .