Mutyambai

NO MORE SECURITY: IG Mutyambai asema walinzi wataondolewa kwa maafisa wakuu waliohusika na uhalifu

Maafisa wa serikali wanaojihusiaha na uhalifu  watapokonywa walinzi ,amesema inspekta mkuu wa Polisi  Hillary Mutyambai .Mutyambai  amesema  wote wanaokabiliwa na kesi kuhusiana na visa mbalimbali vya kukiuka sheria watapokonywa ulinzi wa polisi hadi waondolewe lawamani na mahakama . Mutyambai kupitia taarifa amesema  kwamba watu mashuhuri ambao ni wamiliki wa leseni za kuwa na silaha pia watapokonywa bunduki zao.

NEW MANDATE:Oparanya Achaguliwa mwenyekiti wa CoG bila kupingwa .

” Watu mashuhuri wanaopewa taadhima inayoandaana na vyeo vyao wanafaa kujibu ukarimu huo kwa kuwa watiifu wa sheria  nyakati zote  na wasijuhusishe na vitendo vya kuhujumu dhamira ya kupewa ulinzi wa polisi’ imesema taarifa hiyo. Tangazo hilo linajiri wakati huu ambapo mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino amezuiliwa rumande kwa kumjeruhi DJ mmoja kwa kumpiga risasi shingoni katika eneo la burudani la B Club ijumaa wiki jana .

police letter

 

Photo Credits: radio jambo

Read More:

Comments

comments